Na Nyasigo Kornel
Ni mkoa wa Mara tu uliyobahatika kupakana na nchi tatu za Afrika Mashariki . Angalia kwenye ramani, Mara ipo pembene. Mara ni moja ya mikoa 26 za Tanzania. Musoma ni makao makuu ya mkoa Mara. Musoma ipo sehemu ya kaskasini mwa Tanzania. Ina idadi ya wakazi 1,368,602 ( sensa ya 2002 ),na ni mashariki mwa ziwa Victoria,sio mbali sana na mpaka wa nchi jirani ya Kenya.
Mkoa wa Mara imepakana na mikoa za Mwanza na Shinyanga (kusini), Arusha (kusini mashariki) na Kagera (kupitia ziwa Victoria). Kaskazini mashariki , imepakana na nchi jirani ya Kenya.
Wakazi wa mkoa huu ni wa kabila mbali mbali ikiwemo Wajaluo, Wajita, Waruri, Wazanaki, Wakuria, Wakabwa, Wakiroba, Wasimbiti, Wangoreme, Wakwaya, Waikoma, Wanata, Waisenye, Waikizu, Wasizaki, Wasukuma and Wataturu (Datooga).
Chini ya uongozi wa Uingereza ,Mkoa wa Mara ilikuwa na wilaya,ijulikana kama Lake Province, ambayo ilibadilishwa kuwa Kanda ya Ziwa baada ya uhuru mwaka 1961.
Hifadhi ya wanyama Serengeti , ambayo ni moja kati ya mbuga za wanyama inayotambulika nchini, sehamu yake kubwa ipo mkoa huo wa Mara .Hifadhi hii, yenye sehemu kubwa ya miti na majani mengi ( grasslands and woodlands) ni nyumbani kwa maelfu ya wanyama . Hifadhi ya Serengeti kwa sasa inatambulika kiulimwengu na UNESCO, na inavutia wastani watalii 150,000 kila mwaka.
Inasadikiwa kuwa kuna zaidi ya milioni moja ya mbwa mwitut,Zebra 200,000 na swala 300,000.Mbali na kuwavutia watalii katika hifadhi ya wanyama ya Serengeti, kuna sehemu nyingi sana za kuwavutia .
Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Mara ni Isidori Shirima.
Mkoa wa Mara kuna wilaya za Bunda (kusini magharibi ), Serengeti (kusini mashariki), Tarime na Rorya (kasakazini), naMusoma mjini pamoja na Musoma vijijini.
Rorya , moja ya majimbo mawili ya wilaya ya Tarime imeshatambulika kuwa moja ya wilaya zinzounda mkoa wa Mara. Imepakana na wilaya ya Tarime kwa mashariki, Musoma vijijini kwa kusini, Ziwa Victoria kwa magharibi, na nchi ya Kenya kwa kaskazini . Wengi wa wakazi wa wilaya ya Rorya ni wa kabila la wajaluo. Kabila zingine ni Kurya, Kine, Simbiti na. Suba.
1 comment:
Vema sana.Japo kuna mengi zaidi ya kuzungumzia hasa kwa upande wa wilaya ya Rorya.
Post a Comment