Tuesday, May 29, 2007

Lulu iliyofichika mkoani Mara


Na Nyasigo Kornel


Mto Mara


Mto Mara ni mto katika Afrika unaotirirka katika nchi mbili za Tanzania na Kenya. Mto huu ulipata jina hilo kutokana na hifadhi ya mbuga ya masai Mara iliopo nchini Kenya. Moja ya daraja inayovukisha katika mto huu uitwa Kirumi, ni daraja iliyojengwa kwa ufundi wa hali ya juu huku ikigharimu mabilioni ya pesa, hii pia ni kivutio kikubwa.


Mamba ni wengi sana katika mto huu na hii uletas hamasa ya mtu kufurahia kupiga picha akiwa amesimama kwenye daraja hii au juu ya milima iliyoizunguka daraja hili.


Kisiwa kizuri cha Lukuba inavyopamba mandhari ya Ziwa Victoria
Ikiwa umbali wa kilomita 13 tu kutoka katika ufukwe wa Ziwa Victoria, utaiona kisiwa hiki ukiwa umesimama pemebni mwa ziwa, na uzuri wake uongezeka sana ukiangalia kwa upande wa Makoko Seminari.


Katika kisiwa hiki wamejenga hoteli inayotoa huduma na kuleta madhari ya kuvutia sana, hoteli hii huitwa Lukuba Island Lodge, hoteli hii utoa huduma kwa wasafiri na wale wanaopumzika wakiwa wanaendela na safari.


Ukiwa katika hii huoteli utaona mandhari ya kuvutia sana ya uvuvi wa samaki aina ya chengu na sato.


Hoteli ina majengo tano yaliyoezekwa kwa nyasi inayoleta ladha ya asili na hivyo kuifanya kisiwa kibaki na uasili wake, mawe mazuri ya kun’gaa yameipamba chumba cha chakula huku yakiwa yamezagaa kila eneo la Lukuba.


Hoteli imejengwa chini ya mti mkubwa wa mizeituni iliyozungukwa na mawe aina ya granite iliyobebana kiasi cha kuleta kivutia ya aina yake.


Ukiwa kisiwani hapo, muda wa jioni utaona mamba wengi na kiboko wakiibua vichwa vyao wengine wakiwa wamelalia mawe mazuri ya granite kiasi cha kuwa kivutio kwa wengi.
Ndege weupe wapo kisiwani hapo wakirukaruka bila kuogopa watu, ni ndege wengi kiasi cha kuleta uweupe katika kisiwa hicho kidogo.


Utaona vilevile kenge, gedere, mijusi mikubwa na nyani wengi sana katika kisiwa hiki ambacho akijaharibiwa na shughuli za binadamu.


Kusafiri kuelea katika kisiwa hiki ukuchukua kiasi cha dakika 30-45 kwa boti.
Hoteli hii utoa huduma za boti zenye mawasialano ya radio, GPS, vifaa vya usalama wakati wa hatari na vifaa kama ndoano ya kulowea samaki.


Wageni wengi wanaofika hapa hupenda kuvua samaki wenyewe kwa kutumia ndoano au njia nyingine halali kama njia ya kujifurahisha ukiwa kisiwani hapo.


Hii ni starehe ya aina yake ambayo huwezi ukaipata ukiwa katika hoteli za nchi kavu.



Ziwa Victoria: Nyumba ya sangara

Ziwa Victoria au Viktoria Nyanza ni ziwa kubwa Afrika, pia ni chanzo cha mto Nile, hili ni ziwa la pili kwa ukubwa Duniani.

Ziwa la kwanza ni ziwa Superior ambalo lipo Amerika ya kaskazini, ziwa Victoria lipo futi 3,726 kutoka usawa wa bahari lina eneo la maili za mraba zaidi ya 26,000 maji ya ziwa Victoria yanamiminika kwenye mto Nile na kuelekea bahari ya Mediterenia kwa umbaili wa maili 4,000.

Hata hivyo ziwa Victoria limekuwa ni kiunganisho na mpaka kwa nchi tatu za Afrika ya mashariki ambazo ni Tanzania; Kenya na Uganda.

Uvuvi katika Ziwa Victoria unatoa mchango mkubwa katika kuinua maisha ya wananchi wa mkoa wa Mara na maeneo mengine. Hata hivyo, fursa bado ni kubwa kwa wawekezaji wengi kuwekeza katika eneo hili.


Uvuvi na uuzaji wa samaki, ni shughuli muhimu kwa wakazi wa mkoa wa Mara wanaoishi kandokando ya Ziwa Victoria na mito. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, baadhi ya wakazi wa mkoa huu, wanaishi kwa kutegemea shuhuli za uvuvi katika sehemu kubwa ya maisha yao.


Shughuli hiyo wanaitegemea katika kuwapatia chakula,kukidhi mahitaji muhimu ya maisha, kusomesha watoto wao na hata kufanya shughuli za maendeleo kama vile kujenga nyumba na kuanzisha vitegauchumi hivi na vile.


Kwao uvuvi na samaki ni kila kitu. Shughuli ya uvuvi kwa sasa, ndiyo inayoongoza kwa kuuingizia mkoa huu mapato makubwa ye fedha za kigeni yatokanayo na kodi na ushuru mbalimbali. Uvuvi wa kibiashara unafanywa kwa kutumia vifaa vya kisasa vya uvuvi na maboti. Wavuvi wengi, shughuli zao wanazifanyia katika Ziwa Victoria ambalo linaongoza katika maziwa yanayozalisha samaki wa maji baridi kwa wingi duniani. '


Linatoa zaidi ya asilimia 50 ya samaki wote wanaovuliwa nchini kiasi ambacho ni zaidi ya tani 175,000 kwa mwaka. Kati ya kiasi hicho, zaidi ya asilimia 80 ni samaki aina ya Sangara (Nile perch) ambaye anapatikana katika ziwa hilo pekee duniani. Sangara anashika nafasi ya juu kwenye mazao yanayouzwa kwenye soko la nje. Ziwa hili ambalo lipo katika ardhi ya nchi za Afrika Mashariki, Kenya, Uganda na Tanzania ni mojawapo kati ya maziwa makubwa kabisa duniani likitanguliwa na Ziwa Superior.


Uvuvi katika Ziwa Victoria unatoa mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wa ukanda wa ziwa hili na nchi kwa ujumla. Wakazi wa mkoa wa Mara wanaoishi kando na kwenye visiwa vilivyo katika ziwa hilo, ni vigumu sana kuwatenganisha na shughuli za uvuvi, uuzaji na ulaji wa samaki na dagaa kama kitoweo muhimu katika maisha yao na shughuli ya kibiashara. Kwao ziwa Victoria ni sawa na maisha au uhai. Utamu wa samaki wanaopatikana kwa kuvuliwa katika ziwa hilo, unafahamika vyema sio na wakazi wa mkoa huo tu, ni pamoja na mikoa mengine ya Tanzania na nchi za nje.


Mkoa wa Mara unaongoza kwa uuzaji na usafirishaji samaki nchi za nje. Bado kunahitaji uwekezaji makini katika eneo hili muhimu kwa ajili ya biashara ya samaki,vyakula na mafuta yake. Ziwa Victora lina utajiri mkubwa unaohitaji kuvuliwa na kuendelezwa kwa maslahi ya wananchi na taifa. Shughuli nyingine zinazoambatana na uvuvi ni usafirishaji, uchakataji, uchuuzi wa samaki na uzalishaji viwandani.Maeneo mengine ni ujenzi wa maboti ya uvuvi na mitumbwi. Uvuvi wa samaki kwa wakazi wengi wa mkoa huo, imekuwa kama ni shughuli ya asili,ambayo imefanywa kuwa ya kibiashara katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.


Pia juhudi zitafanywa kuhakikisha uendelevu wa raslimali ya uvuvi ambayo ni zawadi ya kipekee Mungu aliyotupata yawezekana kuwa Ziwa Victoria linaongoza kwa kuingiza mapato.


Mahitaji ya samaki kwa viwanda vinavyosindika, bado ni makubwa hata kusababisha bei yake kupanda kwa wavuvi. Na kwa upande wa walaji wa kawaida majumbani kwa kiasi fulani samaki wamepungua. Kwa hakika mchango wa sekta ya uvuvi katika ajira,lishe na pato la taifa ni mkubwa unafaa kuendelezwa kama tunataka kuona taifa linapiga hatua za uhakika kwa kutimia kikamilifu raslimali zilizopo.



Mbuga ya wanyama ya Serengeti


Mbuga ya wanyama ya Serengeti imetambaa kutoka Kenya hadi Tanzania ikiwa na wanyama wanaohamahama kwa vipindi maalum na hivyo kutangazwa moja ya maajbau saba ya kiutalii duniani.


Jina Serengeti inatokana na neno la kimasai lililo na maana ya nyanda zisizo na mipaka (endless plain).


Mbuga hii ina wanayama wengi sana wapatao milioni mbili

Goldland Hotel:


Katika ardhi hii yenye dhahabu kuna hoteli yenye hiyo hadhi, Goldland Hotel iliyopo kilomita 18 tu kutoka Sirari-Isibania, hutoa huduma bora kabisa ya hoteli huko Tarime. Mazingira ya hoteli hiyo ni ya kuvutia huku kukiwa na vyumba bora, chakula kizuri na huduma ya kisasa katika massive lounge, executive, VIP na presidential suites zilizounganishwa na DSTV pamoja na huduma ya internet.


Ikiwa juu ya kilima Kaskazini Mashariki mwa mji, Goldland Hotel inampa mteja mandhari nzuri ya kuvutia ambayo anaweza kuipata katika miji michache kama Dar es Salaam.


Usiku mmoja tu pale Goldland Hotel will fit nicely into every itinerary and will appeal to those people seeking comfortable lodge-based accommodations in the action packed area of the Tarime.


Mkoa watenga maeneo maalum ya uwekezaji

MKOA wa mara una utitiri wa maeneo ya kuwekeza vitega uchumi

Katika makala hii iliyoandaliwa na Mwandishi LUDGER KASUMUNI, anamnukuu Isidore Leka Shirima –Mkuu wa mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara wa Mkoa wa Mara, akitoa maelezo zaidi juu ya uwekezaji.

“Napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha mkoani Mara, nchi yenye vyanzo vingi vya uwekezaji ukizingatia historia yake na utamaduni uliopevuka.
Kwa mapana yake, fursa kuu za uwekezaji katika mkoa wetu ni zifuatazo;

Mahali ulipo mkoa wa mara ni nguzo na njia kuu ya mtiririko wa biashara katika mikoa ya maziwa makuu.


Ni mahali alipozaliwa Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye ni kiongozi maarufu duniani na ni nyumbani kwa Hifadhi Maarufu ya Wanyama pori ya Serengeti.

Ni mkoa wenye madini mengi hususani gesi aina ya Helium na miamba inayohodhi dhahabu nyingi.


Mara inachukua sehemu kubwa ya pili ya ziwa Victoria katika Afrika Mashariki, ambayo ni nguzo kuu ya uvuvi.


Mkoa una hali ya hewa na ardhi safi kwa uwekezaji katika mashamba makubwa ya biashara ya kilimo, ufugaji, kilimo cha umwagiliaji, ufugaji kwa ajili ya viwanda vya kusindika nyama na maziwa.


Mali asili nyingne ambazo ni muhimu kwa wawekezaji wakubwa kwa maendeleo ya nchi.

Kufuatana na fursa hizi nyingi za uwekezaji, wawekezaji wanaweza kuanzisha vitega uchumi mbalimbali katika nyanja za;

Kilimo cha biashara cha nafaka, mbegu za za kuzalisha mafuta ya kula, maua, mboga za majani, matunda na pamba kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Viwanda vya kusindika bidhaa asilia za mifugo kama vile usindikaji wa nyama kwenye makopo na nyama iliyosagwa kwa matumizi ya binadamu, viwanda vya ngozi na bidhaa za ngozi, machinjio ya kisasa, viwanda vya kuzalisha vyakula vya kuku na wanyama wengine na ranchi za kisasa.

Hoteli za kitalii na huduma za utalii katika mbuga maarufu ya Serengeti.

Utafiti wa madini hususan dhahabu , vito na gesi asilia ya Helium.

Viwanda vya kusindika na kuzalisha bidhaa mbalimbali za samaki. Pia kuna fursa nyingi za kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo (agro-processing industries).

Natumaini kuwa kadri utakavyokaa hapa Mara utaweza kuona vitega uchumi vingi kadri utakavyo kutegemea mahitaji na uwezo wako. Utaweza kuanzisha vitega uchumi kwa ajili ya kuvuna faida na kupunguza umaskini katika jamii inayokuzunguka.

Serikali kuu na ya mitaa mkoani mara ina dhamira ya kuweka mazingira mazuri kabisa ya uwekezaji katika mkoa nuu.

Tafadhali tuunge mkono katika mkakati wa ushirikiano thabiti baina ya sekta binafsi nay a umma ili tuweze kuhakikisha malengo yetu ya maendeleo yanazaa matunda.

FURSA ZIPATIKANO KATIKA MANISPAA YA MUSOMA

Manispaa ya Musoma ilianzishwa rasmi mwaka 1963. Manispaa ina eneo la kilomita za mraba 63. Manispaa hii inapakana na iko sehemu ya ziwa Victoria kwa upande wa mashariki na kaskazini na kwa upande wa kusini na magharibi kuna Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Manispaa hii ina jumla ya wakazi 108,242 kwa mujibu wa sensa ya taifa ya mwaka 2002. Shughuli za uchumi ni kama zifuatazo;

Bandari

Bandari ya Musoma iko upande wa kusini magharibi wa mji. Bandari hii ni muhimu sana kwa usafiri majini hususan kwa kusafirisha abiria na mizigo kati ya Musoma na jiji la Mwanza, Bukoba, Kisumu (Kenya) na Entebbe (Uganda).

Kiwanja cha ndege


Kuna kiwanja kidogo cha ndege chenye vipimo vya kitaalamu vijulikanavyo 1600 x 33 RWY and 60x30 SWY of 0.66. Ndege kama vile aina ya Twin Otter na Fokker 48 hutumia huduma za uwanja huu. Ujenzi wa uwanja mwingine na upanuzi wa uwanja huu utasaidia kutosheleza mahitaji ya abiria na mizigo ya wafanyabishara inayoongezeka kwa kasi. Pia itasaidia kufungua milango ya vituo vya kimataifa vya utalii na biashara katika mkoa huu ambao una rasilimali nyingi. Huduma zitaboresha kulingana na vigezo vya kiusalama wa anga vya kimataifa.

Uvuvi

Kwa kuwa eneo la manispa ya Musoma limezungukwa na ziwa Victoria kiasi cha theluthi mbili, ni eneo muhimu la kuanzisha viwanda vitokanavyo na uvuvi na biashara ya samaki. Kwa hivi sasa manispaa ina viwanda vinner vya kusindika samaki ambavyo ni Mara Fish Park, Musoma Fish Processors, Musoma Fish Filletors na Prime Catch. Lakini bado lipo soko la kuanzisha viwanda vingine zaidi.

Viwanda


Hadi hivi sasa manispaa ina viwanda vichache sana kutokana na kukosekana kwa taarifa muhimu za maeneo ya uwekezaji. Manispaa imeanza kurekebisha kasoro kwa kutenga maeneo maalum ya viwanda vya vidogo vya ukubwa wa kati na vikubwa. Viwanja vimetengwa katika eneo lijulikanalo Kwangwa.

Utalii


Manispaa imekwishajiandaa kuwa mlango vivutio vya utalii vinavyozunguka wilaya ya Musoma ambayo ni Hifadhi maarufu ya Serengeti. Kwa hivi sasa watalii wengi wanatembelea Serengeti kupitia Kenya na Arusha wakati Musoma ni karibu sana na hifadhi hii. Kwa hiyo Musoma ni eneo nzuri sana kwa kuendeleza biashara ya utalii wa kimataifa na hoteli. Maeneo yaliyokwisha pimwa kwa ajili ya ujenzi wa hoteli ni;

-Makoko plot number 201 lenye ukubwa wa mita za mraba 6,998

-Nyabisanye plot number 21 lenye hekta 1.181.
-Bweri plot number 60 lenye hekta 2.66.

Miundombinu

Mitaa na barabara katika Manispaa ya Musoma bado zinatakiwa zipanuliwe na kujengwa upya ili kukidhi mahita yanayoongezeka ua magari, baiskeli na watu waendao kwa miguu. Manispaa imeamua kujenga stendi mpya ya mabasi ya Bweri ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya mji.

Maendeleo ya nyumba na makazi

Huwezi kuwa na maendeleo ya mji bila kujenga nyumba bora kwa ajili ya makazi na biashara. Manispaa imekwishatenga viwanja katika eneo la Kiara plot Na. 448 na Bweri. Maeneo haya yanasubiri wawekezaji kujitokeza.

Asasi za fedha

Biashara haiwezi kukua bila huduma bora za asasi za fedha. Musoma bado inahitaji asasi nyingi na bora zaidi. Hali hii inatoa changamoto kwa manispaa kubuni sheria, taratibu na mikakati ya kuendeleza sekta hii ili ichochee zaidi maendeleo ya uchumi. Hivi sasa manispaa ina asasi zifuatazo:

-CRDB
-NMB
-NBC
-Asasi nyingine za fedha hususan-ushirika wa kuweka na kukopa yaani SACCOS

Kadri milango ya wawekezaji inavyofunguliwa bado kuna soko kubwa la kuanzisha asasi za fedha hapa Musoma.

TARIME, wilaya yenye mazingira mazuri ya uwekezaji

Eneo la kijiografia

Wilaya ya Tarime iko kaskazini mwa Tanzania na iko katika latitudi 1 00" - 1 45" kusini mwa Ikweta na Longitudi 33 30" - 35 0" mashariki mwa Meridian. Wilaya hii ina hali ya ikolojia ya kilimo ya aina tatu ambazo ni nyanda za juu, nyanda za kati na za chini. Nyanda hizi ziko kati ya urefu wa mita 800 na 1,800 kutoka usawa wa bahari. Wilaya hii imepakana na Jamuhuri ya Kenya kwa upande wa kaskazini, wilaya ya Serengeti kwa upande wa mashariki, wilaya ya Musoma kwa upande wa kusini na ziwa Victoria kwa upande wa magharibi.

Eneo:

Wilaya hii ina eneo la kilomita za mraba 11,137, ambazo 3,885 kati ya hizo ni (asilimia 35) za nchi kavu na kilomita za mraba 7,252 zilizosalia ambazo ni (asilimia 65) ni ziwa Victoria. Nchi inayowezakukaliwa na watu ni kilomita za mraba 3,615 na kilomita za mraba 270 ni Hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Idadi ya watu

Kutokana na sensa ya taifa ya watu na makazi ya mwaka 2002, wilaya hii ina watu 490,731. Kiwango cha wastani wa ongezeko la watu ni asilimia 2.8 kati ya mwaka 1988 na 2002. Idadi ya watu hadi kufikia mwaka jana ilikadiriwa kuwa 533,636.

Kilimo:

Ardhi inayofaa kwa kilimo katika wilaya hii ni hekta 192,829, lakini eneo linalolimwa ni wastani wa hekta 130,481. Mazao makuu ya biashara ni kahawa na chai.

Uvuvi:

Shughuli za uvuvi zinachangia asilimia 6.28 ya mapato ya ndani ya wilaya hii.
Masoko makuu ya samaki mara baada ya kuvuliwa wilayani Tarime ni: Sota, Nyang'ombe, Kibuyi, Rwang'enyi na Ruhu. Zana za uvuvi zitumikazo ni, injini za boti, mitumbwi au boti za asili, kafia na nyavu za kuvulia samaki.

Wanyama pori

Wakazi waishio katika vijiji vilivyopakana na hifadhi ya Serengeti wameelimishwa kuhusu umuhimu wa kutunza maliasili na wanyamapori kwa ujumla. Vijiji vinavyonufaika na hifadhi ya Serengeti ni Gibaso, Massanga na Kegonga ambavyo vimenufaika na miradi kadhaa kama vile ujenzi wa charco-dams, madarasa na vituo vya huduma za afya ya msingi. Vijiji vya Gibaso na rito vimekubaliana kuanzisha maeneo tengefu ya hifadhi za maliasili.

Miundombinu

Barabara za lami km 81
Barabara za kokoto km 297
Na barabara za vumbi ni km 422
Jumla ni km 800.

Mawasiliano

Kampuni za simu zinazoendesha biashara wilayani humu
ni Celtel, Vodacom na Tigo. Pia kuna huduma za mawasiliano ya simu na fax zitolewazo na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).
Kilimo

Maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji yamo katika vijiji vifuatavyo:

NA KIJIJI ENEO (HK) Ha
1 Bisarwi Bisarwi Basin 600
2 Nyamirambaro Nyamirambaro 85
3 Bumera Nyerema 250
4 Matongo River Mara Basin 500
5 Kewanja Gonsara 333
6 Kirogo Mori River Basin 500
7 Dett/Ochuna Nyathorogo 875
Jumla Bonde 3,743

Ziwa Victoria ambalo linachukua eneo la kilomita za mraba 7,252 katika wilaya hii ni chanzo muhimu cha kilimo cha umwagiliaji.

Usindikaji wa maziwa

Jedwali hili hapa chini linaonyesha mitambo ya kiwango cha kati kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa:

NA SHAMBA IDADI YA MIFUGO
1 Baraki Sisters 245
2 ICDP Kowak 42
3 UDAFLO
4 MFEC 1221
5 Small Scale
Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa 145

IDADI YA LITA ZA UJAZO ZA MAZIWA
38 82,080
8 23,040
82 180,120
308 1,108800
70 151,200

JUMLA 1,545240

Usindikaji wa chakula

Ndizi huzalishwa kwa wingi katika nyanda za juu. Kitu ambacho wakulima wamekosa ambalo ni tatizo la kudumu ni soko la mazao yao. Kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza uzalishaji wa kilimo ikiwa dhamira ipo.

SERENGETI wilaya yenye hazina kubwa ya utajiri

WILAYA ya Serengeti imepakana na Kenya upande wa kaskazini, wilaya ya Bunda upande wa magharibi na wilaya ya kaskazini magharibi wilaya ya Tarime.

Eneo – Wilaya ina eneo la km 10,373, na kati ya hizo hifadhi ya Serengeti inachukua kilomita za mraba 7000. Pia eneo la kilomita za mraba 183,63 ni mbuga ya Ikorongo, kilomita za mraba 68.37 ni mbuga ya Gurumeti Game Reserve na kilomita za mraba 659 ni kwa ajili ya kilimo, mifugo na makazi ya watu. Kuhusu hali ya hewa wilaya ya Serengeti ina wastani wa joto wa centigredi 26 kwa mwaka.

Kuhusu idadi ya watu, sensa ya mwaka 2002 inaonyesha kuwa wilaya ina wakazi 176,609 na kukua kwa idadi ya watu ni wastani wa asilimia 2.8 kwa mwaka.

Katika nyanja ya kilimo, wilaya hii ina ardhi inayoweza kutumika kwa kilimo kiasi cha hekari 3,600. Katika bonde la mto mara kuna eneo kubwa linaloweza kutumika kwa kilimo cha umwagiliaji.

Gesi ya Helium inapatikana katika kijiji cha Majimoto, ambako kampuni ya Tanzania Oxygen Company ilifanya utafiti na kugundua kuwa kuna miamba yenye gesi nyingi ya Helium.

Mawasiliano: Kampuni mbalimbali za mawasiliano zinaweza kuwekeza katika kutoa huduma za fax, simu za mkononi na landlines katika wilaya hii. Idadi ya watu wanaotaka huduma za mawasiliano katika wilaya hii inaongezeka kila siku hasa kutokana na umaarufu wa hifadhi ya Serengeti.

Utalii

Kwa hivi sasa wilaya ya Serengeti hainufaiki sana na hifadhi ya Serengeti kutokana na ukweli kwamba watalii hawaendi moja kwa moja huko bali hupitia Arusha. Kutokana na hali hii mapato mengi hayawafikii watu wa wilaya hii. Wilaya hii inaweza kuvuta watalii moja kwa moja kutoka Kenya kwani inapakana na Kenya. Hii ni wilaya inayoweza kuunganisha ukanda wa utalii wa Afrika Mashariki vizuri zaidi. Hifadhi ya Serengeti ambayo kwa sasa inaingiza watalii 150,000 kwa mwaka, bado ina uwezo wa kuvuta watalii wengi hususan kwa njia ya utalii wa kiutamaduni. Utalii katika wilaya hii una nafasi kubwa ya kukua lakini bado wawekezaji hawajaweza kuwekeza katika biashara hii. Wawekezaji wanakaribishwa kwa wingi.

Dhahabu:

Hivi sasa kuna shughuli za uchimbaji dhahabu unaoendeshwa na wachimbaji wadogo huko Park Nyigoti, Kilimalambo/Rigwani, Borenga, Rungabure na Majimoto. Sehemu hizo zote zinahitaji uwekezaji na shughuli za utafiti wa madini. Kuna vita aina ya orch na green oxide. Vito hizi zinaweza kupatikana katika kijiji cha Robanda na vito aina ya Quarz zinapatikana katika kijiji cha Rungabure.

Uvuvi – Mto mara ni muhimu kwa ajili ya kuendeleza biashara ya samaki na viwanda vyake kwa kutosheleza mahitaji ya ndani na nje. Mto huu una samaki wengi ambao ni kama vile lungfish, Sato na kadhalika.

Katika nyanja ya usindikaji vyakula kuna uwezekano wa kuanzisha viwanda vya kusindika vyakula kama vile unga wa mahindi, soya na maharage kwa ajili ya mahitaji ya ndani na nje.

Kuhusu usindikaji wa nyama, wilaya ina mifugo mingi kwa ajili ya viwanda vya usindikaji nyama.

Usindikaji wa maziwa pia unaweza kuendelezwa. Wafugaji wanaweza kuzalisha maziwa mengi kwa ajili ya viwanda. Vijiji maarufu kwa kuzalisha maziwa ni Rungabure, Kibachabancha, Ngoreme, issenye, Natta na vingine.

Bidhaa za ngozi pia huzalishwa kwa wingi katika wilaya hii. Kuna uwezekano mkubwa kwa wawekezaji kuzalisha viwanda vya ngozi na bidhaa mbalimbali zitokanazo na ngozi za wanyama. Wilaya hii ina machinjio 17 ambayo huzalisha ngozi karibu kila siku

VIVUTIO NA HAZINA ILIYOKO WILAYANI BUNDA

Baraza la Wilaya ya Bunda ni miongoni mwa mamlaka kuu tano katika mkoa wa Mara. Wilaya ipo kati ya latitudo 1030 na 2045 kusini mwa mstari wa Ikweta na pia kati ya longitudo 33039 na 34005 mashariki mwa mstari wa Griniwichi.

Wilaya ya Bunda imepakana na wilaya ya Musoma Vijijini kwa upande wa kaskazini, wilaya ya Serengeti kwa upande wa mashariki, wilaya ya Magu kwa upande wa kusini na pia imepakana na wilaya ya Ukerewe kwa upande wa magharibi.

Hivyo, Bunda imepakana na wilaya mbili mkoani Mwanza, yaani Magu na Ukerewe.

Wilaya ya Bunda ina eneo la kilometa za mraba 3,088 ambalo ni nchi kavu, huku kilometa za mraba 200 zikiwa katika Ziwa Victoria. Mbuga ya wanyama ya Serengeti inachukua ukubwa wa kilometa za mraba 480, katika eneo la nchi kavu wilayani Bunda.

Shughuli za kiuchumi

Kilimo


Wilaya ina hekta 240,790 za ardhi yenye rutuba, hii ikiwa ni asilimia 83 ya eneo lote la Bunda.
Eneo lililolimwa ni kati ya hekta 50,000 hadi hekta 70,000 ambayo ni sawa na asilimia 20 hadi 30 ya eneo lote linalofaa kwa kilimo. Mazao makuu ya biashara katika wilaya ya Bunda ni pamba, alizeti na ufuta na kunde ambapo pamba huzalishwa kwa wingi zaidi.

Biashara na viwanda

Biashara zinazoendesha wilayani ni pamoja na maduka ya rejareja na jumla, viwanda vitatu vya pamba ambapo viwili kati yake vinazalisha mafuta, pia kuna viwanda viwili vya kutengeneza vifaa vya platic.

Maliasili


Jamii nyingi katika vijiji vinavyoizunguka mbuga wa wanyama ya Serengeti, tayari zimekwisha kuelimishwa na kuhamasishwa juu ya utunzaji wa maliasili kwa ajili ya manufaa ya kizazi kijacho na pia kwa ajili ya uchumi wa taifa.

Wanakijiji hunufaika na mbuga ya Serengeti pamoja na hifadhi ya Grumet kutokana na misaada ya kifedha na nyenzo inayotolewa kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii katika vijiji vyao.

Nyumba za kulala wageni za Kirawira na Grumet pia huchangia mapato katika wilaya ya Bunda ambapo hulipa ada ya kitanda kwa kila mtalii anayepata huduma ya malazi katika nyumba hizo.

Miundo Mbinu

Barabara


Urefu wa jumla wa barabara za kiwango cha chagarawe ni kilometa 692
Barabara kuu zina urefu wa kilometa 99 ambapo kilometa 39 zipo katika kiwang cha lami.
Barabara za wilaya zina urefu wa kilometa 102, huku barabara za ndani maeneo ya vijijini zina urefu wa kilometa 225.
Barabara za maeneo ya mjini zina urefu wa kilometa 60

Huduma za mawasiliano


Huduma za mawasiliano ya simu katika wilaya zinajumuisha mtandao wa simu za ofisini na majumbani [yaani simu za mezani pamoja na fax] ambazo hutolewa na kampuni ya simu (TTCL), pamoja na mtandao wa huduma ya simu za mikononi nchini inayotolewa na makampuni ya tiGO, Celtel na Vodacom. Mashirika ya kidini, jeshi la Polisi na huduma za afya hutumia mawasiliano ya simu za upepo kwa mawasiliano.

Kilimo cha umwagiliaji


Ziwa Victoria ambalo kuchukua eneo la kilometa za mraba 200 katika eneo lote la Bunda, ni hazina na chanzo kikubwa cha maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, ambapo tayari kuna heta 4,150 zinazofaa kwa kilimo hicho cha umwagiliaji.

Maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umagiliaji: Ukubwa
Tamu Nyatwali Hakta 3000
Nyantare Hekta 400
Eneo tambalale la Igundu Hekta 300
Maeneo tambalale ya Karukekere and Muranda Hekta 450

Hivyo jumla ya eneo lote ni hekta 4,150.

Usindikaji wa maziwa


Wafugaji wilayani Bunda huzalisha lita 25,000 za maziwa kwa siku ambazo huuzwa katika viwanda vya usindikaji maziwa. Kiwango hiki cha uzalishaji kujitokeza katika miezi nane tu kwa mwaka ambapo katika kipindi cha miezi minne ya majira ukame, uzalishaji wa maziwa hushuka hadi kufikia lita 10,000 kwa mwezi.

Ufugaji


Ufugaji ni miongoni sekta zinazofanya vizuri katika wilaya ya Bunda. Ufugaji huchangia katika mapato yote ya wilaya kwa asilimia 28, huku karibu asilimia 40 ya kaya zote katika wilaya hujishughulisha na ufugaji. Idadi ya mifugo katika wilaya ni kubwa na hutoa nafasi kubwa zaidi katika uwekezaji. Hivyo, Wilaya in ng’ombe 21,875, mbuzi 76,311, kondoo 47,410, punda 1,225, kuku wa kufuga 182,265 na nguruwe 306.

Ufugaji nyuki


Vijiji sita katika Wilaya hujishughulisha na ufugaji wa nyuki. Vijiji hivyo ni Nyamatake, Mihale, Kihumbu, Mariwanda, Mugeta pamoja na Kyandege, ambapo kuna zaidi ya vikundi 200 vya wafugaji nyuki na pia walinaji asali 811.

Sekta ya Madini


Ingawa hakuna takwimu za kutosha kuhusiana na uchimbaji dhahabu katika Wilaya ya Bunda District; shughuli za uchimbaji mdogo wa dhahabu imekuwa ikiendelea kufanyika katika maeneo ya Buzimbwe, Nyasana, Kamkenga, Karukekere and Kinyambwiga.

Uchimbaji wa kibiashara zaidi ulikuwa ukifanyika wakati wa ukoloni na pia baada ya uhuru katika machimbo ya Kabasa, ambapo uzalishaji ulisimama mnamo mwaka 1967. Aidha, uwepo wa dhahabu katika maeneo haya yaliyotajwa, unakaribisha zaidi jitihada za kufanya uchunguzi wa kitaalam ili kuweza kubaini kama kuna uwezekano wa kuchimba dhahabu kwa malengo ya kibiashara.


MUSOMA, wilaya yenye vivuti vingi vya uwekezaji

Musoma ni moja kati ya Halmashari za Wilaya zilizoko katika Mkoa wa Mara, kaskazini mashariki mwa Tanzania. Wilaya ipo katika pwani ya mashariki mwa Ziwa Victoria na inapakana na Wilaya ya Tarime kwa upande wa kaskazini. Pia, Wilaya ya Musoma inapakana na Wilaya ya Bunda kwa upande wa kusini na vile vile wilaya inapakana na Wilaya ya Serengeti.

Idadi ya watu


Wilaya ya Musoma ina ukubwa wa kilomita za mraba 24,910 ambapo kilometa za mraba 300 ziko ndani ya Ziwa Victoria. Pia, kutokana na takwimu za Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2002, Wilaya ina watu 329,824 huku kasi ya ukuaji wa idadi ya watu ni asilimia 2.5 kwa mwaka.

Sura ya nchi na hali ya hewa


Wilaya ya Musoma ipo katika mita 1,100 hadi 1,500 kutoka usawa wa bahari. Wilaya pia ina sura ya nchi yenye mwambao wa kuvutia unajitokeza hadi katika Ziwa Victoria, mabonde, miinuko ya hapa na pale pamoja na sehemu tambalale zinazotenganishwa na vijito vidogo vinavyoingia ziwani.

Upatikanaji wa mvua na hali ya hewa kwa ujumla hubadilika kutokana na eneo kuwa karibu na ziwa. Kiasi cha mvuani milimita 900 hadi 1200 katika miezi ya Septemba mpaka Disemba na Machi hadi Juni. Hali ya hewa ni joto joto kati ya Sentigredi 24 hadi 32.

Miundo mbinu


Wilaya ya Musoma imeunganishwa vyema na barabara ya lami mpaka katika nchi jirani ya Kenya kupitia wilaya ya Tarime. Pia, Wilaya ya Tarime inaunganishwa na Mkoa wa Mwanza kwa barabara ya lami. Aidha, Musoma inaunganishwa na Mkoa wa Arusha kwa barabara ya changarawe.

Utalii


Musoma ina vivutio vya mandhari mazuri yenye rasi na sehemu ya Ziwa inayoingia nchi kavu upande wa magharibi wa wilaya, eneo la Majita. Sehemu hizi za kuvutia katika mkoa wa Mara ni kama vile Kara na Shirati in kaskazini mwa mkoa.

Katika kisiwa kisichokuwa na watu cha Iriga katika Ziwa Victoria, unaweza kujionea aina mbalimbali za mimea ya kuvutia pamoja na ndege wazuri wasiopatikana katika sehemu nyingine duniani. Katika kisiwa hiki kuna aina ya kipekee ya ng’ombe iliyoletwa katika eneo hilo na watu wasiojulikana. Ng’ombe hao wanafanana na nyati.

Vile vile, unaweza kusafiri kwa gharama nafuu mpaka katika mbuga ya wanyama ya Serengeti, kufurahia mandhari tambalale yenye wanyama wa aina mbalimbali. Pia, Wilaya ina uwanja wa ndege ambao hurahisisha usafiri kwa miji ya Nairobi, Dar es Salaam, Mwanza, au sehemu nyingine yeyote.

Sekta ya madini


Wilaya ya Musoma ina maeneo makubwa yenye utajiri wa dhahabu katika maeneo ya Buhemba, Bisumwa na Etaro. Madini katika maeneo haya bado yanasubiri wawekezaji ili yaweze kufikia hatua ya kuzalisha. Kwa sasa ni kampuni moja tu ndiyo inachimba dhahabu katika eneo la Buhemba.

Uvuvi


Wilaya ya Musoma inakadiriwa kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 100,000 za samaki kwa mwaka lakini wavuvi wadogo waliopo wana uwezo wa kuzalisha tani 30,000 tu za samaki.

Watu wenye zana nzuri za uvuvi wana nafasi nzuri ya kupata soko la uhakika katika viwanda vya kusindika samaki vya jiji la Mwanza na Musoma, mbali na soko la nje ya nchi. Samaki wanatarajiwa kuongezeka katika Ziwa Victoria kutokana na juhudi nziri za vikundi 67 vya wana mazingira vinavyohamasisha uvuvi sahihi usioharibu mazingira.

Katika Wilaya ya Musoma, sehemu inayofaa kwa shughuli za uvuvi ni tarafa ya Mugango iliyopo pembezoni mwa ziwa.

Viwanda vya usindikaji maziwa


Wilaya ya Musoma inazalisha zaidi ya lita milioni 7 za maziwa kwa mwaka. Kwa sasa wilaya haina kiwanda cha kusindika maziwa kutokana na kufungwa kwa viwanda viwili vilivyokuwa vikisindika maziwa vya Nyanka na Makilagi kutokana na matatizo ya kimenejimenti. Viwanda hivi vilikuwa na uwezo wa kusindika lita milioni 2.1 za maziwa kwa mwaka.

Aidha, viwanda vingine vipya vinaweza kuanzishwa, hii ikiwa sambamba na kuvifufua vile vilivyokufa. Kwa wawekezaji wenye nia ya kujenga viwanda vipya, tayari Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imekwisha kutenga eneo linalofaa kwa ajili ya shughuli hiyo katika eneo la kijiji cha Kirumi kilichopo katika eneo la mwinuko, kando kando ya barabara ya lami inayotoka Tarime kuunganisha na Musoma. Barabara hii ina urefu wa nusu kilometa kabla ya kufika katika daraja la Kirumi.

Eneo hili ni zuri kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa kwa kuwa tayari kuna uhakika wa maji kutoka katika Mto Mara au Ziwa Victoria. Pia, kuwapo kwa uhakika wa umeme katika eneo hili pamoja na soko la uhakika katika eneo la ndani na nje ya Mkoa wa Mara, kunalifanya eneo la Kirumi kuwa muafaka zaidi kwa ajili ya uwekezaji.

Viwanda vya kusindika nyama


Wilaya ya Musoma ina zaidi ya ng’ombe 290,000, mbuzi 140,000 na kondoo 34,000. lakini kama pangekuwa na kiwanda cha uhakika cha kusindika nyama, kiwanda hicho kingeweza kujipatia ng’ombe milioni moja kutoka katika wilaya za jirani zilizoko katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga, mbali na wilaya nyingine za Mara. Soko la nyama ya kusindika ni zuri kusafirisha katika nchi jirani za Rwanda, Burundi, Kenya, D.R. Congo, Mashariki ya Kati na kwingineko.

Utengenezaji wa ngozi zitokanazo na mifugo


Wilaya ya Musoma huzalisha ngozi zaidi ya 30,000 kwa mwaka kutokana na ngozi za ng’ombe, kondoo na mbuzi, ambazo husafirishwa nje ya nchi.

Utengenezaji wa chakula cha mifugo


Marighafi ya kutengenezea chakula cha kulishia mifugo hupatikana kwa wingi katika kipindi chote cha mwaka. Marighafi hayo ni mashudu ya mbegu za pamba kutoka viwandani, mifupa ya samaki wa Ziwa Victoria inayobaki baada ya usindikaji wa samaki viwandani, pamoja na mifupa na damu ya mifugo inayopatikana machinjioni.

Hivyo, uhakika wa kupata faida ni mkubwa endapo wawekezaji watajitokeza kujenga viwanda vya kuzalisha chakula cha mifugo kwani soko zuri lipo, ndani na nje ya Mkoa wa Mara.

Mashamba makubwa


Wilaya ya Musoma ina ardhi safi yenye ukubwa wa hekta 13,000 kwa ajili ya mashamba makubwa ya kilimo na ufugaji katika maeneo ya Buhemba, Bugwema and Kiabakari. Ardhi katika eneo la Bugwema iko chini ya Halmashauri ya kijiji wakati ile ya Buhemba na Kiabakari iko chini ya Serikali. Wawekezaji binafsi wanayo fursa kubwa kuwekeza katika nafasi hii kubwa na ya kipekee.

Kilimo kwa ujumla


Ardhi yenye rutuba katika Wilaya ya Musoma ni hekta 398,100. Hata hivyo, ni hekta 132,900 tu, sawa na asilimia 33.3 ndiyo hulimwa kwa mwaka, tena na wakulima wadogo. Hii ina maana ya kuwa, Wilaya haina wakulima wakubwa kabisa.

Aidha, Wilaya ya Musoma bado ina hekta zilizo wazi 265,200 ambazo zinaweza kuchukuliwa na wawekezaji kwenye sekta ya kilimo katika maeneo ya tarafa ya Buswahili kuzunguka eneo la Mto Mara, pamoja na katika tarafa ya Bugwema.

Sekta ya utalii na burudani


Fursa ya kuwekeza ni kubwa katika Wilaya ya Musoma hasa katika sekta ya hoteli. Bado wilaya ina hitaji hoteli za ziada kwani kuna hoteli mbili tu za kiwango cha juu, chenye kuridhisha.




No comments: