Tuesday, May 29, 2007

Kuondoa umaskini ni shughuli za kiroho


Na Nyasigo Kornel

KAMA kuna jambo ambalo wa Anglikana wa jimbo la Mara wanapaswa kujidaia ni mradi huu unaojulikana kama Mogabiri Farmers Extension Centre (MFEC) ambapo ng,ombe wa kisasa wanaotoa maziwa kwa wingi huazimwa kwa mkulima mpaka atakapo zaa. Mkulima hutakiwa kurudisha mradini mtoto aliyezaliwa na kubaki na mama yake.
Kuna aina mbili za ng’ombe wanaotolewa na mradi huu wa MFEC ambao unalenga zaidi kwa familia masikini, nazo ni Frisian na Arson.

Pia kuna shamba la mazao ambako wanawake na wanaume hushiriki sawasawa katika kusafisha eneo, kutayarisha shamba na kupanda wakati shughuli za kupalilia, kuvuna mpaka kuhifadhi mazao hufanywa na wanawake. Wanawake pia wanawajibika katika kuandaa chakula, kuchota maji na kusenya kuni.

Maamuzi katika familia hizi za kikulima hutawaliwa na wanaume hata katika familia ambazo wanawake hutoa mchango mkubwa. Lakini pia bado yapo maamuzi yanayofanywa pamoja.

Kwa watu waishio maeneo ya hifadhi ya taifa ya Serengeti, kuna wakati huamini kuwa hawafaidiki na mbuga hiyo kama ilivyo kuwa zamani kabla sheria kali za kuzuia ujangili hazijawekwa. Lakini wakulima wa matunda na mbogamboga husaidiwa na dayosisi ya Mara kuboresha mazao yao ili kutafuta masoko mapya hususun katika mahoteli ya kitalii yaliyopo katika hifadhi hiyo. Jambo hili huwafanya wajisikie kwa namna Fulani kuwa hifadhi hiyo ni muhimu kwao.

Mradi huu unaodhaminiwa na dayosisi unajulikana jama Mara Small Holders Horticulture Program (MSHHP) upo Bunda.

Dayosisis hii pia ina Integrated Development Program (ICDP) katika vijiji mbalimbali vilivyopo uwanda wa chini wa Mara, na Buhemba Rural Agricultural Centre (BRAC). Vyote hivi ni katika juhudi za kuwawezesha watu kupitia mbinu zao wenyewe.

Dayosisi ya Mara ilianzishwa mwaka 1985 kutoka katika Dayosisi ya Victoria Nyanza. Eneo la Dayosisi ya Mara linachukua eneo zima la Mkoa wa Mara ikipakana na Ziwa Victoria upande wa Magharibi na hifadhi ya Serengeti upande wa Mashariki wakati Kaskazini imepakana na Kenya na mkoa wa Mwanza uko Kusini.

Askofu wa kwanza wa dayosisi hiyo alikuwa Askofu Gershom Nyaronga, na mwaka 1994 askofu wa sasa Hilkiah Omindo lichaguliwa kuchukua nafasi hiyo.

Dayosisi hii ina majimbo manne yenye mapasta 22 sharika 68 na zaidi ya makanisa 200. Inakadiriwa kuwa waumini wa dayosisi hii wanazidi 60,000. Miongoni mwa malengo makubwa ya dayosisi hiyo ni kutua huduma kwa bora kwa jamii ili kuboresha maisha ya watu.Huduma hizo ni pamoja na:
Elimu – Dayosisi ina shule ya sekondari ya Issenye ambayo pia ina zahanati. Pia ina shule ya msingi ya Mara na dayosisi inamiliki chuo cha ufundi.

Kwa upande wa elimu ya kidini, dayosisi ina TEE na Kowak Christian Training Centre, Girls Brigade (ya kwanza hapa nchini) na Christian Resource Centers.

ENDS...

No comments: