Tuesday, May 29, 2007

Kanisa la Mennonite ilinavyoikomboa jamii


Na Nyasigo Kornel


Hospitali ya Shirati ilianzishwa baada ya kuwasili wamisionari kutoka Marekani mwaka 1934. Wamisionari hawa wakwanza wa Mennonite walipania kutoa huduma ya elimu na afya kwa jamii ya Shirati


Baadae wataalamu wa afya madaktari na wauuguzi walipelekwa pale. Taratibu majengo ya kudumu yalijengwa na mwaka 1952 wodi za wanawake na wanaume zilihengwa.
Mwaka 1972 ukarabati mkubwa ulifanyika ili kuweka mandhari ya hospitali katika hadhi ya kisasa.


Katika historia yote, hospitali ya Shirati Hospitali kwa kushirikiana na wamisionari wa kanisa la Mennonite wameendelea kutoa hudum aya afya kwa wote wenye mahitaji hayo.
Serikali imewamba wamisionari hao kufungua chuo kikuu katika hospitali hiyo ambayo kwa sasa inatoa elimu ya uuguzi na wanafunzi kutoka nchini na nchi jirani ya Kenya wanasoma.
Community Mobilization Project (CMP).

Shughuli kubwa ya CMP kwa wa-Mennonite katika dayosisi ya Mara Kaskazini ni kuhamasisha watu kwa kutumia rasilimali walizonazo kushiriki katika shughuli kama kufuga nyuki, samaki katika mabwawa, kulima bustani na kutengeneza majiko yanayotumia nishati kidogo na rafiki wa mazingira.

No comments: